Hali ya Elimu Tanzania
Hali ya Elimu Tanzania Tafiti na Uhalisia vinatuambia nini?
Elizabeth Missokia & Mtemi Zombwe1
1.0 Utangulizi
Katika dunia ya leo, ili kila mtu aweze
kuboresha maisha yake ni lazima awe na elimu. Elimu ndiyo inayomwezesha mtu
kujitambua na kujimiliki yeye mwenyewe kwanza, pia kuzikabili changamoto
zinazomsonga, kuyatawala na kuyatumia mazingira yanayomzunguka ili kuboresha
maisha yake. Ndani ya utandawazi, elimu isiyotosheleza, tafsiri yake ni
umaskini zaidi; wakati elimu zaidi tafsiri yake ni maisha bora zaidi. Nelson
Mandela, Rais mstaafu wa Afrika Kusini amewahi kusisitiza umuhimu wa elimu kwa maendeleo
ya jamii, kwa kusema kuwa; “........elimu ni injini kubwa ya maendeleo ya mtu.
Ni kupitia elimu ndipo binti wa mkulima mdogo anaweza kuwa daktari bingwa,
kwamba mtoto wa kibarua wa mgodini anakuwa Mkuu wa Mgodi, na mtoto wa kibarua
wa mashambani anakuwa Rais wa taifa kubwa”. (Mandela, 1991). Ili elimu iweze
kuleta mabadiliko ya kweli kimaendeleo ni lazima iwe elimu bora-ambayo inalenga
kumbadilisha mtu na kumwezesha kufikiri, kubuni, kujitambua, kuhoji, kudadisi,
kupenda kazi, kuwa na mwenendo mwema na kuboresha afya na maisha yake binafsi
na ya jamii. Elimu ni ukombozi iwapo italenga kumpatia mtu uwezo wa kupambana
na changamato zinazoikabili jamii na taifa kwa ujumla. Elimu inamjenga mtu kuwa
raia makini na mzalishaji ndani ya nchi yake (Zombwe, 2007)
2.0 Historia (kwa ufupi) ya Elimu Tanzania
1 Elizabeth Missokia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu na Mtemi Zombwe ni Mwalimu, Mchambuzi wa Sera
na Mtafiti, HakiElimu. Waandikie kwa info@hakielimu.org au
bettymissokia@yahoo.com/zombwe@gmail.com “Elimu inakuwa na maana sana kama
malengo yake yalikuwa ni kuhakikisha kuwa kipindi wanafunzi wanamaliza shule,
kila mvulana na msichana anapaswa kufahamu kwa kiwango gani hajui, na hivyo
kuhamasika kujenga matamanio ya kutaka kufahamu muda wote maishani mwake” (William
Haley, 1901-1987). Historia ya Elimu nchini inatukumbusha malengo ya msingi ya
elimu Tanzania. Ukiacha elimu ya kibaguzi iliyokuwa inatolewa kabla ya uhuru,
elimu ya Tanzania baada ya uhuru ililenga kumjenga mtu katika nyanja zote ili
awe mzalishaji mzuri katika nchi yake.
Ndio maana elimu na kazi vilisisitizwa sana, na vyuo vya ufundi
pamoja na kazi za mikono vilipewa msisitizo mkubwa, huku suala la usawa, haki
na misingi ya umoja wa kitaifa vikichanua na kushamiri kwenye nyaraka za
serikali na kwenye vichwa vya watu. Dhamira hii ikaleta maboresho makubwa
yakiwemo ongezeko kubwa la uandikishaji, kutaifishwa kwa shule za binafsi na
kufanywa za umma na kuzaliwa kwa Azimio la Arusha lililokuja kua dira ya
kusimamia misingi ya haki, usawa, udugu na utu. Solomon Eliufoo ndiye
aliyeongoza michakato hii kama Waziri wa Elimu kutoka mwaka 1962 hadi 1965.
Katika kipindi chake, Eliufoo alipiga marufuku ada kwa wanafunzi wa sekondari,
kuendeleza ujenzi wa shule za msingi na sekondari na upanuzi wa mafunzo kwa walimu
wa daraja A na C na elimu ya watu wazima.
Pia ndani ya miaka hii mabadiliko mengine tuliyoshuhudia ni
kuruhusiwa kwa Kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia katika elimu ya
msingi na Kiingereza sekondari, kupinga ubaguzi wa rangi katika elimu na elimu
ya msingi kutangazwa kutolewa kwa miaka nane. Kipindi cha 1965 hadi 1970 chini
ya Chediel Mgonja, kilishuhudia maamuzi ya aliyekuwa Rais wa awamu ya kwanza,
Julius Nyerere akitangaza rasmi falsafa mpya ya elimu iliyojulikana kwa jina la
Elimu ya Kujitegemea, kuanzishwa kwa Taasisi ya Elimu na uundwaji wa Baraza la
Mitihani la Afrika Mashariki. Mabadiliko mengine katika kipindi hiki yalihusu
kutungwa kwa Sheria ya Elimu ya mwaka 1969, shule za msingi kufundishwa na
Watanzania pekee na kuimarishwa kwa kisomo cha watu wazima na chenye manufaa.
Elimu ya watu wazima ndiyo iliyojenga nchi na kuiweka kwenye hadhi ya juu
katika medani za kimataifa, hasa kwenye suala la upunguzaji wa ujinga.
Hadi kufikia mwaka 1986 kiwango cha watanzania kujua kusoma na
kuandika kilikuwa ni asilimia 91, tofauti na sasa kimeshuka hadi asilimi 692.
Miaka ya 1975 hadi 1980 ilishuhudia mabadiliko mengi tu kwenye mfumo wa elimu
yetu. Ni kati ya miaka hiyo Ujenzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi
ulifanyika, kutolewa kwa Tamko la Elimu ya Msingi kwa wote, ujenzi wa vituo vya
ufundi kwa wahitimu wa elimu ya msingi na kuzuiwa kwa mtihani wa darasa la nne.
Pia Taasisi ya Ukuzaji Mitaala na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima zilianzishwa.
Na mwaka 1978 ndicho kipindi ilipotungwa Sheria ya Elimu namba 25 chini ya
Waziri Nicholas Kuhanga. Kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, mengi yamefanyika
ikiwemo kuanza kwa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP), kuanza kwa
Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo wa Elimu
ya Sekondari (MMES).
Mipango hii ndiyo
inayoshika hatamu za kuiendesha elimu yetu kuelekea kwenye ubora na fursa sawa
kwa wote. Je, tija ya mabadiliko haya toka uhuru ina mwelekeo gani kwa taifa?
Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umasikini, (MKUKUTA), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi(MMEM), Mpango wa
Maendeleo 2 Taarifa ya idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika aliyoitoa
Naibu Waziri wa Elimu, Philip Mulugo; bungeni tarehe 15 februari 2011 ya Elimu
ya Sekondari(MMMES) na Sera ya Elimu na Mafunzo vyote vinabainisha ukweli huu
kuwa ili Tanzania ipige hatua kali za kimaendeleo ni lazima wananchi wake
wapate elimu bora iliyokamilika. Lakini je, elimu inayotolewa hapa Tanzania,
inakidhi haya yote? Ama ni kwa kiasi gani inawawezesha watoto na vijana kufikia
malengo hayo? Hili ndilo swali la msingi linalopaswa kutuongoza kuelekea kwenye
mipango na vitendo vinavyoipeleka mbele elimu yetu na siyo kuirudisha nyuma.
2.0 Mafanikio ni mengi. Tumepiga hatua kubwa! Tanzania imeweza kupiga hatua
kubwa kwenye utaoji elimu kwa wananchi wake. Kwa kupitia MMEM, MMES na MEMKWA;
watoto wengi wa Kitanzania wamepata fursa ya kujiunga na elimu ya msingi na
sekondari.
Hadi mwaka 2010 zaidi ya watoto milioni 8 (ambao ni zaidi ya 90%
ya uandikishaji halisi) wameandikishwa shule za msingi na zaidi ya wanafunzi 1,
638, 699 wako sekondari. (Tazama chati namba 1) Chanzo: BEST 2001 & 2010
Idadi ya shule na walimu imeongezeka maradufu. Hadi mwaka 2010 shule za
sekondari zimeongezeka kutoka shule 937 na kufikia idadi ya 4,2663 mwaka 2010.
Walimu nao wameajiriwa kwa idadi kubwa ili kusaidia mchakato wa kuwapatia
watoto elimu. Kwa mfano, hadi mwaka 2010 idadi ya walimu wa shule za msingi na
sekondari imefikia walimu 206, 3734 kutoka idadi ya walimu 54,869 mwaka 2001.
Ongezeko hili limechangiwa na ongezeko kubwa la wanafunzi kwa kuanzia miaka ya
2001 hadi 2010.(tazama jedwali na 1). Hii ni dhahiri kuwa fursa za elimu kwa
wote zimeongezeka nchini, na hatuna budi kuipongeza serikali na wadau wa elimu
kwa jitihada hizo.
3.0 Tafiti zinatuambia nini?
Licha ya mafanikio haya ni dhahiri kuwa
elimu yetu bado inakabiliwa na changamoto nyingi. Tafiti na tathmini za
serikali5, vyuo vikuu, wanaharakati na mashirika binafsi zinabainisha ukweli
huo, ambao ni muhimu kuuzingatia ili kutafuta majibu kwa pamoja. Uchambuzi huu
mfupi haudai kuchambua na kutoa ufumbuzi wa matatizo yote, bali kwa kiasi
kuchambua na kuchangia mapendekezo ambayo yatakuwa mchango katika kuleta
mabadiliko. Baadhi ya changamoto kubwa kwenye elimu yetu ni hizi:
3.1 Dira ya elimu: Kuna mkanganyiko wa
uelewa wa nini maana ya elimu, ambapo watanzania tumekosa dira ya pamoja
inayoelekeza ni elimu ya aina gani tunayotaka watoto wetu wapate. Tafiti nyingi
ikiwemo ule wa HakiElimu, uliofanyika mwaka 2007, zimebainisha kuwa kuna uelewa
tofauti wa nini maana na malengo ya elimu nchini. Wananchi wengi waliohojiwa
walisema kuwa elimu ni kuwa na vitendea kazi vya kutosheleza kama vile vitabu,
majengo, madawati na vifaa vya kufundishia. Wengine walielezea elimu ni kujua
kiingereza, na wengine walidai elimu ni uwezo wa kufaulu mtihani tu. Huku ni
wachache sana (chini ya 20%) waliweza kuelezea kwa mapana zaidi na kutoka nje
kidogo ya vitendea kazi kwa kueleza kuwa, elimu ni uwezo, maarifa, ujuzi na
mabadiliko anayopata mtu baada ya kujifunza. Kulingana na mtazamo huu wananchi
wengi wameendelea kuhimizwa kufanya bidii zaidi kwenye kujenga majengo na
kuzipendezesha shule, kulipia watoto tuisheni kuliko kuweka mkazo na kufuatilia
nini mtoto anajifunza pale darasani. Na kwa sababu hizi, tulio wengi
tumeendelea kuhesabu viwango vya ufaulu mitihani kuwa ndio elimu, badala ya
uwezo na ujuzi waliopata, na kufanya hivyo watoto wanaendelea kuambulia matupu
kwenye baadhi ya shule nyingi. Yaani, wanamaliza shule bila hata kujua kusoma
na kuandika (Uwezo, 2011).
3.2 Lugha ya kufundishia: Lugha ya
Kiingereza kama lugha ya kufundishia sekondari imeendelea kuwa kikwazo kikubwa,
ambacho kimechangia katika kushindwa kuelewa masomo kwa umakini darasani.
Utafiti wa HakiElimu wa mwaka 2007 ulibaini zaidi ya 60% ya wanafunzi wa sekondari
hawajui lugha hii ya Kiingereza kwa ufanisi na walishindwa kusoma ama kutafsiri
aya rahisi ya kiingereza iliyoandaliwa kwa ngazi ya darasa la pili. Na
wanafunzi wa shule ya msingi hali ni mbaya zaidi, karibu 75% walishindwa kusoma
aya rahisi ya darasa la pili. Na matokeo ya hivi karibuni ya Utafiti wa Uwezo6,
yanaonesha watoto 7 kati 10 wenye umri kati ya miaka 5-16 wanashindwa kusoma
aya rahisi ya Kiingereza ya darasa la pili. Na kwa sababu shule za sekondari
lugha ya kujifunzia na ya mitihani ni Kiingereza, huwezi kutarajia mwanafunzi
asiyejua Kiingereza kuelewa masomo darasani na hatimaye kufaulu 5 Kama
ufuatiliaji wa Matumizi ya fedha za umma (PETS) 2009, Mapitio ya utekelezaji wa
MMEM, MMES na Ripoti za Mkaguzi na Mdhibti Mkuu wa Hesabu za Serikali,
zinabainisha madhaifu mengi kwenye mfumo wetu wa elimu. 6 Uwezo ni mradi wa
kupima stadi za msingi za kujua kusoma, kuandika na kuhesabu. Uko chini ya
Asasi ya TEN/MET. Utafiti wao wa kwanza umefanyika wilaya 40 za Tanzania bara
mwezi Aprili 2010. mtihani. Pia siyo siri, kuwa hata baadhi ya walimu wetu pia
wanapata shida sana kufundisha kwa lugha ya Kiingereza, kwani walimu pia ni
matunda ya mfumo huu huu wa elimu. Na bila shaka kushuka kwa ufaulu kwenye
mitihani ya kidato cha nne mwaka 2010 (nusu ya wanafunzi wote waliofanya
mtihani walipata daraja sifuri7) kumechangiwa na wanafunzi kutojua lugha hasa
kwenye shule za kata. Lugha ya kujifunzia na kufundishia ni muhimu sana kwa
wanafunzi na walimu kuweza kuilewa kikamilifu, ili kuwawezesha kuwasiliana na
kujifunza. Lugha inaweza kuwa kikwazo kikubwa katika kuchangia kushuka kiwango
cha elimu iwapo wanafunzi hawataimudu, maana watashindwa kupokea maarifa
kikamilifu na wao kushindwa kujieleza ipasavyo. Hali na mwenendo wa matokeo ya
kidato cha nne inaleta picha ya kufikirika. Tazama mchoro hapo chini
unaolinganisha matokeo ya kidato cha nne kwa miaka 10. Chanzo: Takwimu za NECTA
2001-2010 7 Taarifa ya Matokeo ya Baraza la mitihani,
3.3 Kama matokeo ya kidato cha nne
mwaka 2010 yanaonesha watoto wetu 88% wamepata daraja la nne na sifuri. Na pia
Naibu Waziri wa Elimu hivi bungeni alisema Watanzania 31%8 hawajui kusoma na
kuandika. Huu ni USHAHIDI TOSHA kuwa bado jitihada za ziada zinahitajika
kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye dimbwi la UJINGA. (tazama chati namba 6).
Ongezeko la wanafunzi wanaopata daraja sifuri, linakwenda sambamba na ongezeko
la watu wasiojua kusoma na kuandika. Ukilinganisha takwimu vitu hivi viwili
vina uhusiano wa karibu sana. 8 Majira Februari 15, 2011. 0 kutokana na
kupunguza kwa kasi idadi ya wananchi wake wasio jua kusoma na kuandika. Chini
ya Sera ya Elimu ya watu wazima, nchi iliongeza idadi ya watu wanaojua kusoma
na kuandika kila kukicha. Na manufaa yake yalionekana bayana maana watu
waliweza kupambana na changamoto zinazowakabili. Lakini pia waliongeza
uzalishaji mashambani na kuongeza uelewa wa kujikinga na maradhi na magonjwa
mbalimbali. Hadi kipindi Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani, idadi ya
watanzania waliokuwa hawajui kusoma na kuandika ilikuwa takribani asilimia 9 tu.
Hivyo, tungeweza kwenda na mwenendo huo hadi mwaka 2010 tungekuwa na angalau
95% ya watanzania wanaojua kusoma na kuandika. Na tungebaki tunafikiria mambo
makubwa ya ugunduzi, uvumbuzi viwanda na teknolojia ya hali ya juu. Kuongezeka
kwa idadi ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika ni ushahidi kuwa tunarudi
nyuma badala ya kusonga mbele.
3.4 Uhaba wa walimu hasa katika masomo
ya hisabati na sayansi: Asili ya masomo ya sayansi na hisabati ni mantiki,
kutafiti, kufikiri na kuchambua. Hivyo, ni ngumu sana kukariri masomo haya na
kufaulu mtihani. Uhaba wa walimu kwenye masomo haya umetajwa karibu sehemu zote
kuwa ni chanzo kikubwa cha ufaulu duni wa wanafunzi. Na kwa sababu masomo haya
hayakaririki wanafunzi ni ama wapate walimu wa kuwafundisha wenye uwezo au
wafeli mitihani yao. Na kwa sababu sayansi ni msingi mzuri wa teknolojia na
uvumbuzi hasa kwa dunia ya leo ya utandawazi, wanafunzi kukosa walimu kwenye
11% 31% 89% 69% 0% 20% 40% 60% 80% 100% Mwaka 1986 Mwaka 2010 Chati 7: Asilimia
ya idadi ya watanzania wanaojua na wasiojua kusoma na kuandika Wasiojua kusoma
Wanaojua kusoma masomo hayo inakuwa changamoto kubwa kwa nchi kwani uzalishaji
utakuwa duni na hatuwezi kuendeleza teknolojia ndani ya nchi yetu. Tutasubiri
tu teknolojia za kuletewa!
3.5 Uwezo mdogo wa baadhi ya walimu na
motisha ndogo kwao inachangia kuwafanya washindwe kuwasaidia watoto kwa viwango
tarajiwa. Walimu wenye uwezo duni wamekuwa wakisema wazi kuwa hawawezi
kufundisha masomo fulani. Na wale wanaolazimishwa kufundisha masomo hayo wengi
huyafundisha bila kuleta tija. Wanaingia darasani wanajaza ubao lakini watoto
hawaelewi, na hawajifunzi. Hivyo, ujifunzaji unakuwa mdogo sana na wakati
fulani haupo kabisa kwa watoto japo walimu wanaingia darasani na kufundisha. Na
kutokana na baadhi ya walimu kukosa hisia za kazi na motisha kwenye
ufundishaji, hawajitumi, kujiendeleza na wala kuwa wabunifu wa namna ya
kuwasaidia watoto kujifunza. Wanafanya kazi kwa mazoea tu. Kwa mwalimu, hamasa
ya ndani na hisia za kufundisha ndio msingi wa ualimu ambao unajengwa na
saikolojia ya walimu. Walimu wanaaminiwa kuwasaidia watoto kuutambua ukweli
ndani ya dunia ili kuibua vipaji na vipawa vyao. Hili kwa sasa ni changamoto
kubwa!
3.6 Ucheleweshaji wa ruzuku kwa
wanafunzi nalo linatajwa karibu katika kila utafiti kuwa ni tatizo kubwa ndani
ya mfumo wetu wa elimu. Ruzuku kwa kila mwanafunzi ni fedha inayomtunza mtoto
shuleni, kwa kununulia mahitaji yake ya msingi katika usomaji kama vitabu na
chaki. Lakini katika shule nyingi fedha ya ruzuku kwa wanafunzi hazifiki kama
inavyotakiwa, zinachelewa kufika shule. Na kwenye baadhi ya shule fedha
hazifiki kwa kiasi kilichopangwa au kinachohitajika. Hivyo, walimu wakuu
wamekuwa katika wakati ngumu wa kupanga namna ya kuzitumia fedha kidogo
zinazofika ilihali wanafunzi wakiongezeka kila kukicha. Mathalani, Fedha za
rukuzu kwa mwanafunzi kwa mujibu wa MMEM ni Sh 10,000 kwa kila mwanafunzi elimu
ya msingi, lakini kutokana na tafiti za hivi karibuni fedha inayofika shuleni
ni wastani wa Sh 5000. Kwa sekondari kati ya Sh 25,000 zinazopaswa kupelekwa ni
wastani wa sh 7500 ndizo hufika shuleni9. Kwa mwendo huu ni vigumu sana kupiga
hatua (Tazama chati namba 8) 9 Takwimu za MOVET-PETS, 2009 na HakiElimu
PETS-2010 zinabainisha ukweli huo
3.7 Mitaala ya sasa haikidhi mahitaji
ya jamii pana. Wananchi wanatarajia mwanafunzi akifundishwa mabadiliko
yaonekane bayana. Pia aweze kujimudu maisha yake pindi anapomaliza shule. Hili
ndio tegemeo la wengi. “...Mimi nafikiri lengo kubwa la elimu ni kurithisha
vizazi vyetu na vizazi vijavyo, maarifa, ujuzi, na stadi za maisha ili mtu
anapotoka shuleni aweze kujitegemea kuendesha maisha yake wakati wowote na
popote kuendana na mabadiliko” (Mzazi, Monduli, 2010)
3.8 Mabadiliko ya mitaala ya mara kwa
mara ni kikwazo kikubwa cha utoaji elimu bora: Walimu na wanafunzi walibainisha
hili kwa kina. Mabadiliko yanapotokea ya mtaala, vifaa au vitabu havifiki na
wakati fulani unakosa hata kitabu kimoja kinachoendana na mtaala mpya. Na
vinapopatikana huchelewa sana kuwafikia walengwa. Walimu wanakosa la kufanya.
Wanabaki wanasubiri huku watoto wanaelekea kwenye mitihani wakiwa hawajui kitu.
Ilitolewa mfano kuwa kwa mwaka 2010, mpaka kufikia mwezi wa nane, darasa la
sita walikuwa hawana hata kitabu kimoja kwa baadhi ya masomo ambayo yalihusisha
mabadiliko yaliyohitaji vitabu vipya.
3.9 Uelewa mdogo wa masuala ya elimu:
Baadhi ya wananchi vijijini, hasa jamii za wafugaji, na wakulima walio
pembezoni mwa nchi yetu bado hawana ulewa wa kina juu ya masuala mbalimbali ya
elimu na hata umuhimu wa elimu kwa watoto wao. Hivyo, kutojua tu masuala ya
elimu kwa ujumla ni changamoto. Maana wazazi hawawezi kufuatilia watoto
wanajifunza nini. Na baadhi ya wazazi walidai hawawezi kufuatilia ujifunzaji wa
watoto wao maana hawajui Kiingereza, ambacho ndiyo lugha wanayoandika watoto
wao kwenye 0 0 0.2 0.4 0.6 0.8 1 Basic Salary Deduct PPF Ruzuku (Sh.bilioni)
Chati 8: Tofauti kati ya ruzuku halisi iliyofika wilayani na Iliyopaswa kufika
wilayani kwa mujibu wa MMEM II. vitabu. Lakini pia wazazi walidai
hawashirikishwi na walimu, ili kuweza kufuatilia maendeleo ya elimu ya watoto
wao, hivyo hawajui waanzie wapi. (HakiElimu, 2009)
3.10 Vifaa vya maabara na vifaa vya
sayansi bado ni changamoto kubwa maeneo mengi. Walimu wanaandaa masomo ya
sayansi na kuyafundisha bila kuwa na vifaa vya kufanyia hivyo. Na baadhi ya
vifaa hata vikipelekwa shuleni walimu hawajui kuvitumia wala kufundishia
wanafunzi. Kwa sehemu kubwa walimu na wanafunzi walisema hakuna maabara, na
hiki ni kikwazo kikubwa katika kufundishia masomo ya sayansi. Ni vigumu sana
kufundisha masomo kama Biolojia, Kemia na Fizikia bila maabara na vifaa vyake.
Wanafunzi10 walisema kwa kejeli kwamba hata “Bunsen burner” wanaijua kwa picha
tu, lakini ngumu kabisa ni kujua matokeo ya uchanganyaji wa kemikali mbalimbali
kwa njia ya kufikirika!
3.11 Walimu wengi kukosa mafunzo ya
ualimu kazini. Wengi wanashindwa kumudu kazi zao vizuri kwa sababu ya kukosa
mafunzo hayo. Hasa walimu wa leseni ambao waliletwa kwa lengo la kusaidia kutoa
elimu huku wakijiendeleza. Udhaifu wa walimu umezaa tatizo jingine pia la
walimu kukataa baadhi ya masomo wanayopewa kufundisha. Na kutokana na hilo
masomo kama Hisabati na Sayansi yana upungufu mkubwa wa walimu. Swala hili
lilikuwa la utata kiasi kwani wakati, wilayani maafisa elimu waliripoti kuwa
mafunzo kazini yamekuwa yakifanyika mara kwa mara, lakini kwa walimu wengi
waliohojiwa walikanusha na kushangaa kuhusu suala hili.
3.12 Uhaba wa vitabu na uwepo wa vitabu
vya kiada vya waandishi tofautitofauti hasa shule za msingi unaathiri elimu
nchini Tanzania. Maana wanafunzi wanachanganywa na uwingi wa vitabu hivyo. Na
kibaya zaidi, vitabu hivyo vingi vina makosa. Kwa hiyo, kwa watoto wadogo
wakifundishwa dhana moja kitofauti ni lazima watachanganyikiwa na kupoteza
dira. Lakini kwa wilaya za vijijini suala kubwa ni uhaba wa vitabu vyenyewe
kwenye maeneo mengi. Wauza vitabu na wasambazaji hawapeleki vitabu vyote, ni
baadhi tu vitafika wilaya za pembezoni. Hali hii inasababisha baadhi ya shule
kutoweza kupata baadhi ya vitabu hasa ambavyo wanaamini ni vizuri zaidi kwenye
maudhui na uchambuzi wa mada. Na kwa sababu mtihani unatungwa mmoja nchi nzima,
kutokuwa na usawa katika mgawanyo wa vitabu kunawapa faida ya upendeleo
wanafunzi wa mijini wanaopata vitabu, na hivyo wanakuwa kwenye nafasi nzuri
kufaulu zaidi mitihani kuliko walioko shule za vijijini.
3.13 Wingi wa masomo shule za msingi ni
tatizo kubwa kwenye baadhi ya maeneo yenye upungufu wa walimu na vifaa. Yaani
mwanafunzi anakuwa na mzigo mkubwa na akimaliza 10 Sehemu ya mahojiano na
wanafunzi katika shule mbalimbali za wilaya ya Monduli katika utafiti wa
mahusiano kati ya ubora wa mitaala na elimu bora, Agosti 2010 hapo anakuwa hana
stadi nyingi anazozimudu ili zimsaidie kujitegemea katika maisha. Walimu
wanaona ni vyema huko mbeleni wanafunzi waelekezwe kwenye masomo machache tu na
kwenye taaluma ambayo watakwenda nayo hadi ngazi za juu kisha itawasaidia
kufanikiwa maishani. Ndivyo wanavyofanya wenzetu walioendelea. (Mtemi,
2011).
4.0 Tufanye nini ili tuboreshe elimu yetu?
Upatikanaji wa elimu bora unategemea
mambo mengi sana, lakini, hapa tumejaribu tu kutaja mambo muhimu machache, kama
mapendekezo ambayo yanaweza kuchangia kutoa dira. Uwepo wa mitaala bora na
nyenzo bora za kufundishia na kujifunzia pamoja na ushiriki wa wadau muhimu
katika michakato ya maendeleo na utekelezaji wa mtaala ni mambo muhimu sana ya
kuzingatiwa. Utafiti wa HakiElimu na mashirika mengine, ikiwepo serikali pia
umebaini kwamba shule nyingi hapa nchini hazina nyenzo bora za kufundishia na
kujifunzia. Na mtaala wa taifa haukidhi tena mahitaji ya jamii pana. Ili
kuboresha michakato ya maendeleo na utekelezaji wa mtaala, mapendekezo
yafuatayo yametolewa:-
4.1 Mitaala yetu inapaswa kuboreshwa
ili ishabihiane na mahitaji ya jamii kubwa na mabadiliko makubwa yanayoendelea
kutokea. Wananchi wengi wanaonekana kutaka kurudi kwenye mtaala unaoendana na
elimu ya kujitegemea11, ili wahitimu waandaliwe kujitegemea na kumudu
changamoto ndani ya jamii yao, hata kama watakosa fursa za kuendelea mbele
waweze kuishi maisha ya ustawi. Wananchi na hata wanafunzi shuleni, wangependa
kuona vijana wanapatiwa mafunzo ambayo yatawapatia ujuzi na maarifa ili waweze
kujiajiri na kushiriki katika shughuli za kilimo, ufundi, biashara kwa kutumia
mbinu za kisasa na za kuleta tija.
4.2 Wananchi wengi wanadai kuwa mfumo
wa matumizi ya vitabu vya aina nyingi hauna tija kwa kuwa unawafanya wanafunzi
wajifunze dhana zinazotofautiana wakati wakitarajiwa wafanye mtihani wa aina
moja12. Kwa mfano, iwapo kitabu kimoja kitasema, ini ni sehemu ya ubongo na
kitabu kingine kikasema ini linapatikana tumboni maana yake ni kwamba watoto
watakuwa wanachanganywa. Hii ni kuwadanganya watoto ukizingatia ukweli kwamba
upatikanaji wa vitabu hivi hauko sawa (baadhi watapata A, wengine watapata B), lakini
wote wanatarajiwa kufanya mtihani wa aina moja na wanatarajiwa kutoa majibu
sahihi. Kwa kuwa Tanzania tumeamua kuwa na mtihani mmoja nchi zima, basi ni
vema tukawa na vitabu ambavyo vinapatikana kwa usawa kwa shule zote, ili
ushindani nao uwe wa usawa. 11 Elimu ya kujitegemea chini ya utawala wa Nyerere
ndiyo iliyopandikiza fikra za watanzania kupenda kufanyakazi na kufanyakazi kwa
ujumla. 12 Utafiti wa HakiElimu: Mahusiano kati ya ubora wa mitaala na Ubora wa
Elimu, 2011
4.3 Wananchi wengi, wazazi, walimu na
wanafunzi walipendekeza matumizi ya vitabu vya aina moja, hasa shule za msingi.
Na kwa hiyo serikali inapaswa kuliangalia hili kwa faida ya wote na ili
kuhakikisha kuwa kunakuwa na elimu bora na inayotolewa kwa usawa. Kwa hiyo,
kuna haja ya kuifanyia marekebisho sera ya matumizi ya vitabu vya kiada iliyopo
kwa sasa ili iwe kama ilivyokuwa zamani ambapo kitabu cha aina moja chenye
ubora kilikuwa kinatumika nchi nzima.
4.4 Ubora katika vitabu ni jambo nyeti
na la muhimu sana. Vitabu ndiyo kiongozi kikubwa kwa walimu na wanafunzi hivyo
waandishi wa vitabu hivi lazima wazingatie ubora na ukweli wa mambo. Wakati
soko huria la utengenezaji na usambazaji wa vitabu lililenga kupunguza uhaba
mkubwa wa vitabu, kuna haja ya kudhibiti ubora wa vitabu ili kuhakikisha kuwa
vitabu vinavyopendekezwa kutumika mashuleni vinakuwa na ubora unaohitajika. Kwa
sasa utafiti unaonesha, vitabu vinavyochapishwa na wachapishaji mbalimbali
vinatofautiana sana kwa ubora na kwamba baadhi ya vitabu havina ubora
unaohitajika.
4.5 Ushiriki wa wazazi na wanajamii
katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala ni suala muhimu katika kufanikisha
kitendo cha ujifunzaji kwa wanafunzi. Kwa sasa ushiriki wa wazazi na wanajamii
katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala ni mdogo hapa nchini. Kuna haja ya
kuchukua hatua madhubuti, kwanza kuwahamasisha wazazi na viongozi katika jamii
juu ya umuhimu wa ushiriki wao katika maendeleo ya watoto wao shuleni. Pili,
suala la mabadiliko ya mtaala ni sharti lizingatie maoni ya wadau wote muhimu
ukijumuisha wazazi, walimu, wanafunzi na wanajamii wengine. Walimu na wazazi
wana mchango mkubwa katika elimu na ni lazima wawe na uwezo wa kuchangia
masuala mbalimbali ya elimu likiwemo la utunzi wa mitaala kwa nafasi na kiwango
chao cha ujuzi. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa “wale wenye wajibu wa
kufanya na vijana wa umri mdogo, wana nguvu kubwa zisizozidiwa na nguvu za
yeyote yule kwa kutilia maanani hali ya baadaye ya jamii yetu. Nguvu hizi ziko
katika makundi mawili, wazazi na walimu” (Agosti 27, 1966).
4.6 Matumizi ya Kiingereza kama lugha
ya kufundishia katika shule za sekondari inaonekana kama kikwazo kikubwa katika
ushiriki wa wazazi katika kuwasaidia watoto wao kwa kuwa wazazi wengi hawaimudu
lugha hiyo. Suala la lugha ya kufundishia limekuwa likiibua mijadala mizito na
kwamba mwafaka umekuwa haufikiwi katika suala hili. Kuna haja kwa Serikali
kuchukua hatua madhubuti katika kuongoza majadiliano kuhusu lugha ya
kufundishia katika mfumo wetu wa elimu ili kufikia muafaka. Watoto hujifunza
vizuri zaidi iwapo wataimudu lugha ya kufundishia, vivyo hivyo kwa walimu
wakati wa kufundisha. Suala hili linapaswa kutazamwa kwa makini zaidi ili
kuhakikisha kuwa lugha ya kufundishia inafahamika vyema kwa walimu na
wanafunzi.
4.7 Ukosefu wa nyenzo na vifaa vya kufundishia
na kujifunzia ulionekana kama kikwazo katika utekelezaji wa mtaala. Tatizo hili
ni kubwa zaidi kwa vitabu vya sayansi na maabara. Ukosefu wa nyenzo hizi za
kufundishia na kujifunzia hauwezi kupuuzwa kwa kuwa umebainishwa pia kwenye
tafiti zilizopita. Kuna haja kwa wasimamizi katika sekta ya elimu kutilia mkazo
suala la upatikanaji wa nyenzo za kutosha za kufundishia na kujifunzia katika
shule zetu kwa kuwa bila upatikanaji wa nyenzo hizo muhimu ufanisi katika
utekelezaji wa mtaala hautakuwepo. Wengi walikiri kuwa serikali imeamua jambo
jema kupanua fursa za watoto wengi kupata elimu ya msingi na sekondari. Lakini
waliongeza kusema kuwa, ni muhimu pia shule hizi ziwe bora na ni bora sasa
kuboresha shule zilizopo na kuziwekea walimu wa kutosha, kuboresha mazingira ya
kujifunzia, vifaa na vitabu, badala ya kuendelea kujenga shule nyingi ambazo
hazina mafanikio. Tunarudia tena kunukuu maneno ya busara ya Mwalimu Nyerere,
aliyewahi kusema kwamba, “.....tunaposema kupanua elimu ya sekondari,
tunaharakisha sana kusema kwamba, watu watachangia ujenzi kwa juhudi zao,
lakini majengo hayana umuhimu wa kwanza, ...vitu muhimu katika elimu ni walimu,
vitabu kwa sayansi ni maabara” (The situation and Challenges of Education
inTanzania, Nyerere 1984)
4.8 Utekelezaji wenye ufanisi katika
mtaala hutegemea mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia. Wanafunzi wengi
walioshiriki katika utafiti walikosoa mazingira ya ujifunzaji. Japokuwa walimu
walipongezwa na wanafunzi wengi, bado mazingira yao ya kazi ni magumu kwa kuwa
wanafundisha madarasa makubwa, kuna ukosefu wa nyenzo za kufundishia, nyumba
zao za kuishi siyo bora, mishahara yao ni midogo na hawapati mafunzo ya mara
kwa mara. Kuna haja kwa wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili kuboresha
mazingira ya kujifunzia kwa watoto na hatimaye kuwafanya watoto wawe na furaha,
wawe salama. Shule inapaswa kuwa sehemu ambayo itawafanya watoto wafanikiwe
kitaaluma na kimaisha. Hakuna ubishi kwamba, walimu wengi wamekata tamaa na
ualimu imekuwa ni sehemu tu ya waliokosa, hivyo ni vema nchi ifanye jitihada za
makusudi kurejesha upya hadhi na taaluma ya ualimu.
4.9 Mafunzo kwa walimu: Kama
kweli tunahitaji elimu bora hatuwezi kukwepa kuandaa walimu bora. Na walimu
bora wanatokana na msingi bora wa mafunzo bora ya kutosheleza na yanayoendana
na mtaala na dira za maendeleo za nchi. Walimu wakiandaliwa hovyohovyo watatoa
elimu ya hovyohovyo-na hatimaye tutakuwa na wasomi wa hovyohovyo-wanaofanya
kazi hovyohovyo na kuwa na maendeleo duni. Muda wa mafunzo kwa walimu tarajali lazima
uwe kamilifu. Wakufunzi wao lazima wawe bora, na mafunzo kwa walimu kazini
lazima yafanyike kwa ukamilifu wake bila kuleta visingizio vingi. Kama sekta
nyingine wanapata semina, kozi fupifupi kwanini walimu wasipate hivyo. Hakuna
njia ya mkato. Ili fedha inayotengwa na serikali kwenye elimu ilete tija basi
mafunzo ya walimu ni muhimu ili kuandaa watekelezaji wazuri wa sera ya elimu.
Na kwa sababu tayari Serikali ina Mkakati wa Usimamizi na Maendeleo ya Walimu
(TDMS), ni muhimu mkakati huu utekelezwe kwa vitendo kama ulivyopangwa ili
kusaidia kupunguza na hata kuondoa kabisa tatizo la walimu.
4.10 Siasa – Ni lazima wanasiasa
watambue kuwa sekta ya elimu siyo sehemu wala jukwaa lao la kuoneshana umahiri
wa kuongea na kutoa maamuzi hata yanayotupeleka kuzimu. Wakati ni muhimu sana
kwa viongozi wetu kuwa wabunifu na kuleta mawazo bunifu kuboresha sekta ya
elimu, lakini pia wakumbuke wizara ya elimu inakuwa na mipango na bajeti yake
kama wizara nyingine. Kabla ya kutoa maagizo kwa mashindano, ni lazima kuwe na
uratibu na utekelezaji wa sera kikamilifu. Na mawazo ya kisiasa yazingatie na
kufikiria athari za maagizo yasiyo na tija katika elimu. Mambo ya kitaalamu
kuhusu elimu yashauriwe na wataalamu hasa walimu.
4.11 Kuna mgawanyo usio sawa wa
rasilimali za taifa hasa kwenye elimu. Shule za mijini zinaonekana kupendelewa
kwa kila hali. Tafiti nyingi zinaonesha walimu wenye sifa wengi hupangwa
mijini. Bado, hata mgawo wa ruzuku kwa wanafunzi shule za vijijini zinaonekana
kupata kiasi na mara nyingi fedha zinachelewa kuliko shule za mjini13. Hii sio
sawa. Watanzania wengi wako vijijini. Hivyo, ni lazima kuwe na mgawanyo sawa
unaozingatia haki za watoto wote wa Tanzania.
4.12 Kushangilia matokeo ya mitihani
zaidi badala ya ujuzi na maarifa sio sahihi. Kila mtu anapenda kufanikiwa na
kusifiwa, ndiyo hulka yetu binaadamu na hili si kosa. Watanzania tumeacha
kushangilia tija sasa tunashangilia kufaulu mtihani, bila kujali tunapataje
mafanikio hayo, kwa kuiba mitihani, ama kuweka mkazo mwaka wa mwisho tu (darasa
la saba na Kidato cha nne) katika kufundisha. Tunapoteza nguvu nyingi sana
kufundisha watahiniwa ili wafaulu mitihani na kutaka wilaya ama shule zetu
ziongoze kwenye ufaulu , badala ya kutumia muda mwingi kuwasaidia watoto kupata
maarifa, ujuzi na ubunifu ili uwasaidie maishani.
4.13 Kwa nini tusijiulize swali,
kwanini baadhi ya watoto wetu wanafaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari
lakini hawajui kusoma na kuandika vizuri? Je hii ni elimu na mafanikio ya
kushangilia? Elimu siyo cheti, bali ni uwezo, kama mwalimu Nyerere alivyowahi
kusema, 13 MOVET –PETS 2009 na HakiElimu PETS 2010 ..“kinyume kabisa na elimu,
ni aina ya mafunzo inayomfundisha mtu kujifananisha na bidhaa, ambazo thamani
yake inapimwa kwa vyeti, shahada, au sifa nyingine za kitaaluma”(Nyerere 20 Mei
1974)
4.14 Kiuhalisia, elimu ya kweli
hupatikana kwenye mchakato unaoendelea kati ya mwalimu na mwanafunzi darasani.
Hivyo, mbinu za kufundishia na vitendo vya ujifunzaji vinapaswa viboreshwe
kikamilifu. Kazi za kujifunza darasani na mbinu za kuibua vipaji na kuchagiza
maarifa ni muhimu viboreshwe. Na walimu wanapaswa kuwa na hamasa ya kufanya
hivyo ili tupate manufaa ya haraka.
4.15 Mazingira mazuri ya kazi ndicho
kigezo muhimu zaidi kinachoamua kiwango cha moyo wa kujitolea walio nao walimu
katika kufundisha, na matokeo yake kigezo hiki huwa na nguvu sana katika kuleta
matokeo mazuri ya wanafunzi kitaaluma. Bila kurekebisha hili uwekezaji mkubwa
katika elimu hautaleta tija katika taaluma ya ualimu na elimu kwa ujumla
4.16 Mwalimu kuwa na sifa nzuri za
kitaaluma pekee yake bila moyo wa kujitolea haitosho kuimarisha ufaulu wa
mwanafunzi. Shule zenye walimu wenye moyo wa kujitolea wa hali ya juu bila
kujali iwapo walikuwa na sifa za juu kitaaluma (shahada au zaidi) au la
zilifanya vizuri katika mitihani ya taifa. Jitihada mahsusi zifanyike kurejesha
hamasa, kujituma na moyo wa kufundisha.
4.17 Serikali na wadau wengine
washirikiane kuboresha mazingira ya kazi na makazi ya walimu. Usimamizi thabiti
kuhakikisha kuwa walimu wanatimiza wajibu wao, hii itasaidia kujituma zaidi na
kuleta ufanisi katika kazi. Maslahi ya walimu yaboreshwe, na pia walimu
wapandishwe madaraja na kulipwa stahili zao bila kucheleweshwa; hii itachangia
kurejesha hamasa. Na Mafunzo kwa walimu kazini ya uongozi kwa wakuu na
wasimamizi wa shule yatolewe kwa ukamilifu na mara kwa mara, kwani yatasaidia
sana kuongeza ufanisi na ufundishaji wa walimu
4.18 Vigezo vitumike bila
upendeleo au woga kuhakikisha kwamba kila shule inafikia viwango
vinavyokubalika ndiyo ifunguliwe na iendeshwe kama shule; shule ziwezeshwe
kufikia viwango hivi; na zile ambazo zitashindwa kwa kipindi kilichokubaliwa
zisiruhusiwe kuendelea ‘kupotosha’ ama ‘kupotezea’ muda wanafunzi. Zifungwe
kama zinavyofungwa zahanati zisizofikia viwango kubalifu.
4.19 Jitihada mahsusi za baadhi ya
walimu zitambuliwe na walimu hao watuzwe ili kuwatia moyo, na kuwahamasisha
wengine kufanya kazi yao kwa bidii. Kujituma na kuwajibika ni sehemu muhimu ya
maadili ya walimu, hivyo inawapasa walimu wote nchini wazingatie hili; hata
kama wakiwa na hoja ama madai mengine ya msingi.
5.0 Hitimisho
Nchi haiwezi kuendelezwa na watu
wachache wanaopata fursa za kipekee kwenye shule chache huku elimu ya jamii
pana ikiwa mashakani. Hakuna haja kulumbana wala kuingiza siasa katika elimu,
bali serikali itekeleze mipango na sera zilizopo na kuboresha mapungufu kwa
kushirikisha wadau. Na ukweli wa hali ya elimu nchini usisulubiwe wala kubezwa
bali tuupokee na kuuwekea mikakati kwa pamoja tuweze kuboresha elimu yetu. Pa
kuanzia ni kila mmoja katika eneo lake, na kikubwa kufanya zaidi ya mazoea.
No comments:
Post a Comment