Friday, 3 June 2016

Hali ya Elimu Tanzania

Hali ya Elimu Tanzania

Hali ya Elimu Tanzania Tafiti na Uhalisia vinatuambia nini? 


Elizabeth Missokia & Mtemi Zombwe1



 1.0 Utangulizi 

Katika dunia ya leo, ili kila mtu aweze kuboresha maisha yake ni lazima awe na elimu. Elimu ndiyo inayomwezesha mtu kujitambua na kujimiliki yeye mwenyewe kwanza, pia kuzikabili changamoto zinazomsonga, kuyatawala na kuyatumia mazingira yanayomzunguka ili kuboresha maisha yake. Ndani ya utandawazi, elimu isiyotosheleza, tafsiri yake ni umaskini zaidi; wakati elimu zaidi tafsiri yake ni maisha bora zaidi. Nelson Mandela, Rais mstaafu wa Afrika Kusini amewahi kusisitiza umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya jamii, kwa kusema kuwa; “........elimu ni injini kubwa ya maendeleo ya mtu. Ni kupitia elimu ndipo binti wa mkulima mdogo anaweza kuwa daktari bingwa, kwamba mtoto wa kibarua wa mgodini anakuwa Mkuu wa Mgodi, na mtoto wa kibarua wa mashambani anakuwa Rais wa taifa kubwa”. (Mandela, 1991). Ili elimu iweze kuleta mabadiliko ya kweli kimaendeleo ni lazima iwe elimu bora-ambayo inalenga kumbadilisha mtu na kumwezesha kufikiri, kubuni, kujitambua, kuhoji, kudadisi, kupenda kazi, kuwa na mwenendo mwema na kuboresha afya na maisha yake binafsi na ya jamii. Elimu ni ukombozi iwapo italenga kumpatia mtu uwezo wa kupambana na changamato zinazoikabili jamii na taifa kwa ujumla. Elimu inamjenga mtu kuwa raia makini na mzalishaji ndani ya nchi yake (Zombwe, 2007)

2.0 Historia (kwa ufupi) ya Elimu Tanzania 

1 Elizabeth Missokia ni Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu na Mtemi Zombwe ni Mwalimu, Mchambuzi wa Sera na Mtafiti, HakiElimu. Waandikie kwa info@hakielimu.org au bettymissokia@yahoo.com/zombwe@gmail.com “Elimu inakuwa na maana sana kama malengo yake yalikuwa ni kuhakikisha kuwa kipindi wanafunzi wanamaliza shule, kila mvulana na msichana anapaswa kufahamu kwa kiwango gani hajui, na hivyo kuhamasika kujenga matamanio ya kutaka kufahamu muda wote maishani mwake” (William Haley, 1901-1987). Historia ya Elimu nchini inatukumbusha malengo ya msingi ya elimu Tanzania. Ukiacha elimu ya kibaguzi iliyokuwa inatolewa kabla ya uhuru, elimu ya Tanzania baada ya uhuru ililenga kumjenga mtu katika nyanja zote ili awe mzalishaji mzuri katika nchi yake.
Ndio maana elimu na kazi vilisisitizwa sana, na vyuo vya ufundi pamoja na kazi za mikono vilipewa msisitizo mkubwa, huku suala la usawa, haki na misingi ya umoja wa kitaifa vikichanua na kushamiri kwenye nyaraka za serikali na kwenye vichwa vya watu. Dhamira hii ikaleta maboresho makubwa yakiwemo ongezeko kubwa la uandikishaji, kutaifishwa kwa shule za binafsi na kufanywa za umma na kuzaliwa kwa Azimio la Arusha lililokuja kua dira ya kusimamia misingi ya haki, usawa, udugu na utu. Solomon Eliufoo ndiye aliyeongoza michakato hii kama Waziri wa Elimu kutoka mwaka 1962 hadi 1965. Katika kipindi chake, Eliufoo alipiga marufuku ada kwa wanafunzi wa sekondari, kuendeleza ujenzi wa shule za msingi na sekondari na upanuzi wa mafunzo kwa walimu wa daraja A na C na elimu ya watu wazima.
Pia ndani ya miaka hii mabadiliko mengine tuliyoshuhudia ni kuruhusiwa kwa Kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia katika elimu ya msingi na Kiingereza sekondari, kupinga ubaguzi wa rangi katika elimu na elimu ya msingi kutangazwa kutolewa kwa miaka nane. Kipindi cha 1965 hadi 1970 chini ya Chediel Mgonja, kilishuhudia maamuzi ya aliyekuwa Rais wa awamu ya kwanza, Julius Nyerere akitangaza rasmi falsafa mpya ya elimu iliyojulikana kwa jina la Elimu ya Kujitegemea, kuanzishwa kwa Taasisi ya Elimu na uundwaji wa Baraza la Mitihani la Afrika Mashariki. Mabadiliko mengine katika kipindi hiki yalihusu kutungwa kwa Sheria ya Elimu ya mwaka 1969, shule za msingi kufundishwa na Watanzania pekee na kuimarishwa kwa kisomo cha watu wazima na chenye manufaa. Elimu ya watu wazima ndiyo iliyojenga nchi na kuiweka kwenye hadhi ya juu katika medani za kimataifa, hasa kwenye suala la upunguzaji wa ujinga.
Hadi kufikia mwaka 1986 kiwango cha watanzania kujua kusoma na kuandika kilikuwa ni asilimia 91, tofauti na sasa kimeshuka hadi asilimi 692. Miaka ya 1975 hadi 1980 ilishuhudia mabadiliko mengi tu kwenye mfumo wa elimu yetu. Ni kati ya miaka hiyo Ujenzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi ulifanyika, kutolewa kwa Tamko la Elimu ya Msingi kwa wote, ujenzi wa vituo vya ufundi kwa wahitimu wa elimu ya msingi na kuzuiwa kwa mtihani wa darasa la nne. Pia Taasisi ya Ukuzaji Mitaala na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima zilianzishwa. Na mwaka 1978 ndicho kipindi ilipotungwa Sheria ya Elimu namba 25 chini ya Waziri Nicholas Kuhanga. Kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, mengi yamefanyika ikiwemo kuanza kwa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP), kuanza kwa Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari (MMES).
 Mipango hii ndiyo inayoshika hatamu za kuiendesha elimu yetu kuelekea kwenye ubora na fursa sawa kwa wote. Je, tija ya mabadiliko haya toka uhuru ina mwelekeo gani kwa taifa? Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini, (MKUKUTA), Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi(MMEM), Mpango wa Maendeleo 2 Taarifa ya idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika aliyoitoa Naibu Waziri wa Elimu, Philip Mulugo; bungeni tarehe 15 februari 2011 ya Elimu ya Sekondari(MMMES) na Sera ya Elimu na Mafunzo vyote vinabainisha ukweli huu kuwa ili Tanzania ipige hatua kali za kimaendeleo ni lazima wananchi wake wapate elimu bora iliyokamilika. Lakini je, elimu inayotolewa hapa Tanzania, inakidhi haya yote? Ama ni kwa kiasi gani inawawezesha watoto na vijana kufikia malengo hayo? Hili ndilo swali la msingi linalopaswa kutuongoza kuelekea kwenye mipango na vitendo vinavyoipeleka mbele elimu yetu na siyo kuirudisha nyuma. 2.0 Mafanikio ni mengi. Tumepiga hatua kubwa! Tanzania imeweza kupiga hatua kubwa kwenye utaoji elimu kwa wananchi wake. Kwa kupitia MMEM, MMES na MEMKWA; watoto wengi wa Kitanzania wamepata fursa ya kujiunga na elimu ya msingi na sekondari.

Hadi mwaka 2010 zaidi ya watoto milioni 8 (ambao ni zaidi ya 90% ya uandikishaji halisi) wameandikishwa shule za msingi na zaidi ya wanafunzi 1, 638, 699 wako sekondari. (Tazama chati namba 1) Chanzo: BEST 2001 & 2010 Idadi ya shule na walimu imeongezeka maradufu. Hadi mwaka 2010 shule za sekondari zimeongezeka kutoka shule 937 na kufikia idadi ya 4,2663 mwaka 2010. Walimu nao wameajiriwa kwa idadi kubwa ili kusaidia mchakato wa kuwapatia watoto elimu. Kwa mfano, hadi mwaka 2010 idadi ya walimu wa shule za msingi na sekondari imefikia walimu 206, 3734 kutoka idadi ya walimu 54,869 mwaka 2001. Ongezeko hili limechangiwa na ongezeko kubwa la wanafunzi kwa kuanzia miaka ya 2001 hadi 2010.(tazama jedwali na 1). Hii ni dhahiri kuwa fursa za elimu kwa wote zimeongezeka nchini, na hatuna budi kuipongeza serikali na wadau wa elimu kwa jitihada hizo.

3.0 Tafiti zinatuambia nini? 
Licha ya mafanikio haya ni dhahiri kuwa elimu yetu bado inakabiliwa na changamoto nyingi. Tafiti na tathmini za serikali5, vyuo vikuu, wanaharakati na mashirika binafsi zinabainisha ukweli huo, ambao ni muhimu kuuzingatia ili kutafuta majibu kwa pamoja. Uchambuzi huu mfupi haudai kuchambua na kutoa ufumbuzi wa matatizo yote, bali kwa kiasi kuchambua na kuchangia mapendekezo ambayo yatakuwa mchango katika kuleta mabadiliko. Baadhi ya changamoto kubwa kwenye elimu yetu ni hizi: 

3.1 Dira ya elimu: Kuna mkanganyiko wa uelewa wa nini maana ya elimu, ambapo watanzania tumekosa dira ya pamoja inayoelekeza ni elimu ya aina gani tunayotaka watoto wetu wapate. Tafiti nyingi ikiwemo ule wa HakiElimu, uliofanyika mwaka 2007, zimebainisha kuwa kuna uelewa tofauti wa nini maana na malengo ya elimu nchini. Wananchi wengi waliohojiwa walisema kuwa elimu ni kuwa na vitendea kazi vya kutosheleza kama vile vitabu, majengo, madawati na vifaa vya kufundishia. Wengine walielezea elimu ni kujua kiingereza, na wengine walidai elimu ni uwezo wa kufaulu mtihani tu. Huku ni wachache sana (chini ya 20%) waliweza kuelezea kwa mapana zaidi na kutoka nje kidogo ya vitendea kazi kwa kueleza kuwa, elimu ni uwezo, maarifa, ujuzi na mabadiliko anayopata mtu baada ya kujifunza. Kulingana na mtazamo huu wananchi wengi wameendelea kuhimizwa kufanya bidii zaidi kwenye kujenga majengo na kuzipendezesha shule, kulipia watoto tuisheni kuliko kuweka mkazo na kufuatilia nini mtoto anajifunza pale darasani. Na kwa sababu hizi, tulio wengi tumeendelea kuhesabu viwango vya ufaulu mitihani kuwa ndio elimu, badala ya uwezo na ujuzi waliopata, na kufanya hivyo watoto wanaendelea kuambulia matupu kwenye baadhi ya shule nyingi. Yaani, wanamaliza shule bila hata kujua kusoma na kuandika (Uwezo, 2011). 

3.2 Lugha ya kufundishia: Lugha ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia sekondari imeendelea kuwa kikwazo kikubwa, ambacho kimechangia katika kushindwa kuelewa masomo kwa umakini darasani. Utafiti wa HakiElimu wa mwaka 2007 ulibaini zaidi ya 60% ya wanafunzi wa sekondari hawajui lugha hii ya Kiingereza kwa ufanisi na walishindwa kusoma ama kutafsiri aya rahisi ya kiingereza iliyoandaliwa kwa ngazi ya darasa la pili. Na wanafunzi wa shule ya msingi hali ni mbaya zaidi, karibu 75% walishindwa kusoma aya rahisi ya darasa la pili. Na matokeo ya hivi karibuni ya Utafiti wa Uwezo6, yanaonesha watoto 7 kati 10 wenye umri kati ya miaka 5-16 wanashindwa kusoma aya rahisi ya Kiingereza ya darasa la pili. Na kwa sababu shule za sekondari lugha ya kujifunzia na ya mitihani ni Kiingereza, huwezi kutarajia mwanafunzi asiyejua Kiingereza kuelewa masomo darasani na hatimaye kufaulu 5 Kama ufuatiliaji wa Matumizi ya fedha za umma (PETS) 2009, Mapitio ya utekelezaji wa MMEM, MMES na Ripoti za Mkaguzi na Mdhibti Mkuu wa Hesabu za Serikali, zinabainisha madhaifu mengi kwenye mfumo wetu wa elimu. 6 Uwezo ni mradi wa kupima stadi za msingi za kujua kusoma, kuandika na kuhesabu. Uko chini ya Asasi ya TEN/MET. Utafiti wao wa kwanza umefanyika wilaya 40 za Tanzania bara mwezi Aprili 2010. mtihani. Pia siyo siri, kuwa hata baadhi ya walimu wetu pia wanapata shida sana kufundisha kwa lugha ya Kiingereza, kwani walimu pia ni matunda ya mfumo huu huu wa elimu. Na bila shaka kushuka kwa ufaulu kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2010 (nusu ya wanafunzi wote waliofanya mtihani walipata daraja sifuri7) kumechangiwa na wanafunzi kutojua lugha hasa kwenye shule za kata. Lugha ya kujifunzia na kufundishia ni muhimu sana kwa wanafunzi na walimu kuweza kuilewa kikamilifu, ili kuwawezesha kuwasiliana na kujifunza. Lugha inaweza kuwa kikwazo kikubwa katika kuchangia kushuka kiwango cha elimu iwapo wanafunzi hawataimudu, maana watashindwa kupokea maarifa kikamilifu na wao kushindwa kujieleza ipasavyo. Hali na mwenendo wa matokeo ya kidato cha nne inaleta picha ya kufikirika. Tazama mchoro hapo chini unaolinganisha matokeo ya kidato cha nne kwa miaka 10. Chanzo: Takwimu za NECTA 2001-2010 7 Taarifa ya Matokeo ya Baraza la mitihani, 

3.3 Kama matokeo ya kidato cha nne mwaka 2010 yanaonesha watoto wetu 88% wamepata daraja la nne na sifuri. Na pia Naibu Waziri wa Elimu hivi bungeni alisema Watanzania 31%8 hawajui kusoma na kuandika. Huu ni USHAHIDI TOSHA kuwa bado jitihada za ziada zinahitajika kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye dimbwi la UJINGA. (tazama chati namba 6). Ongezeko la wanafunzi wanaopata daraja sifuri, linakwenda sambamba na ongezeko la watu wasiojua kusoma na kuandika. Ukilinganisha takwimu vitu hivi viwili vina uhusiano wa karibu sana. 8 Majira Februari 15, 2011. 0 kutokana na kupunguza kwa kasi idadi ya wananchi wake wasio jua kusoma na kuandika. Chini ya Sera ya Elimu ya watu wazima, nchi iliongeza idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika kila kukicha. Na manufaa yake yalionekana bayana maana watu waliweza kupambana na changamoto zinazowakabili. Lakini pia waliongeza uzalishaji mashambani na kuongeza uelewa wa kujikinga na maradhi na magonjwa mbalimbali. Hadi kipindi Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani, idadi ya watanzania waliokuwa hawajui kusoma na kuandika ilikuwa takribani asilimia 9 tu. Hivyo, tungeweza kwenda na mwenendo huo hadi mwaka 2010 tungekuwa na angalau 95% ya watanzania wanaojua kusoma na kuandika. Na tungebaki tunafikiria mambo makubwa ya ugunduzi, uvumbuzi viwanda na teknolojia ya hali ya juu. Kuongezeka kwa idadi ya wananchi wasiojua kusoma na kuandika ni ushahidi kuwa tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele. 

3.4 Uhaba wa walimu hasa katika masomo ya hisabati na sayansi: Asili ya masomo ya sayansi na hisabati ni mantiki, kutafiti, kufikiri na kuchambua. Hivyo, ni ngumu sana kukariri masomo haya na kufaulu mtihani. Uhaba wa walimu kwenye masomo haya umetajwa karibu sehemu zote kuwa ni chanzo kikubwa cha ufaulu duni wa wanafunzi. Na kwa sababu masomo haya hayakaririki wanafunzi ni ama wapate walimu wa kuwafundisha wenye uwezo au wafeli mitihani yao. Na kwa sababu sayansi ni msingi mzuri wa teknolojia na uvumbuzi hasa kwa dunia ya leo ya utandawazi, wanafunzi kukosa walimu kwenye 11% 31% 89% 69% 0% 20% 40% 60% 80% 100% Mwaka 1986 Mwaka 2010 Chati 7: Asilimia ya idadi ya watanzania wanaojua na wasiojua kusoma na kuandika Wasiojua kusoma Wanaojua kusoma masomo hayo inakuwa changamoto kubwa kwa nchi kwani uzalishaji utakuwa duni na hatuwezi kuendeleza teknolojia ndani ya nchi yetu. Tutasubiri tu teknolojia za kuletewa! 

3.5 Uwezo mdogo wa baadhi ya walimu na motisha ndogo kwao inachangia kuwafanya washindwe kuwasaidia watoto kwa viwango tarajiwa. Walimu wenye uwezo duni wamekuwa wakisema wazi kuwa hawawezi kufundisha masomo fulani. Na wale wanaolazimishwa kufundisha masomo hayo wengi huyafundisha bila kuleta tija. Wanaingia darasani wanajaza ubao lakini watoto hawaelewi, na hawajifunzi. Hivyo, ujifunzaji unakuwa mdogo sana na wakati fulani haupo kabisa kwa watoto japo walimu wanaingia darasani na kufundisha. Na kutokana na baadhi ya walimu kukosa hisia za kazi na motisha kwenye ufundishaji, hawajitumi, kujiendeleza na wala kuwa wabunifu wa namna ya kuwasaidia watoto kujifunza. Wanafanya kazi kwa mazoea tu. Kwa mwalimu, hamasa ya ndani na hisia za kufundisha ndio msingi wa ualimu ambao unajengwa na saikolojia ya walimu. Walimu wanaaminiwa kuwasaidia watoto kuutambua ukweli ndani ya dunia ili kuibua vipaji na vipawa vyao. Hili kwa sasa ni changamoto kubwa! 

3.6 Ucheleweshaji wa ruzuku kwa wanafunzi nalo linatajwa karibu katika kila utafiti kuwa ni tatizo kubwa ndani ya mfumo wetu wa elimu. Ruzuku kwa kila mwanafunzi ni fedha inayomtunza mtoto shuleni, kwa kununulia mahitaji yake ya msingi katika usomaji kama vitabu na chaki. Lakini katika shule nyingi fedha ya ruzuku kwa wanafunzi hazifiki kama inavyotakiwa, zinachelewa kufika shule. Na kwenye baadhi ya shule fedha hazifiki kwa kiasi kilichopangwa au kinachohitajika. Hivyo, walimu wakuu wamekuwa katika wakati ngumu wa kupanga namna ya kuzitumia fedha kidogo zinazofika ilihali wanafunzi wakiongezeka kila kukicha. Mathalani, Fedha za rukuzu kwa mwanafunzi kwa mujibu wa MMEM ni Sh 10,000 kwa kila mwanafunzi elimu ya msingi, lakini kutokana na tafiti za hivi karibuni fedha inayofika shuleni ni wastani wa Sh 5000. Kwa sekondari kati ya Sh 25,000 zinazopaswa kupelekwa ni wastani wa sh 7500 ndizo hufika shuleni9. Kwa mwendo huu ni vigumu sana kupiga hatua (Tazama chati namba 8) 9 Takwimu za MOVET-PETS, 2009 na HakiElimu PETS-2010 zinabainisha ukweli huo 

3.7 Mitaala ya sasa haikidhi mahitaji ya jamii pana. Wananchi wanatarajia mwanafunzi akifundishwa mabadiliko yaonekane bayana. Pia aweze kujimudu maisha yake pindi anapomaliza shule. Hili ndio tegemeo la wengi. “...Mimi nafikiri lengo kubwa la elimu ni kurithisha vizazi vyetu na vizazi vijavyo, maarifa, ujuzi, na stadi za maisha ili mtu anapotoka shuleni aweze kujitegemea kuendesha maisha yake wakati wowote na popote kuendana na mabadiliko” (Mzazi, Monduli, 2010) 

3.8 Mabadiliko ya mitaala ya mara kwa mara ni kikwazo kikubwa cha utoaji elimu bora: Walimu na wanafunzi walibainisha hili kwa kina. Mabadiliko yanapotokea ya mtaala, vifaa au vitabu havifiki na wakati fulani unakosa hata kitabu kimoja kinachoendana na mtaala mpya. Na vinapopatikana huchelewa sana kuwafikia walengwa. Walimu wanakosa la kufanya. Wanabaki wanasubiri huku watoto wanaelekea kwenye mitihani wakiwa hawajui kitu. Ilitolewa mfano kuwa kwa mwaka 2010, mpaka kufikia mwezi wa nane, darasa la sita walikuwa hawana hata kitabu kimoja kwa baadhi ya masomo ambayo yalihusisha mabadiliko yaliyohitaji vitabu vipya. 

3.9 Uelewa mdogo wa masuala ya elimu: Baadhi ya wananchi vijijini, hasa jamii za wafugaji, na wakulima walio pembezoni mwa nchi yetu bado hawana ulewa wa kina juu ya masuala mbalimbali ya elimu na hata umuhimu wa elimu kwa watoto wao. Hivyo, kutojua tu masuala ya elimu kwa ujumla ni changamoto. Maana wazazi hawawezi kufuatilia watoto wanajifunza nini. Na baadhi ya wazazi walidai hawawezi kufuatilia ujifunzaji wa watoto wao maana hawajui Kiingereza, ambacho ndiyo lugha wanayoandika watoto wao kwenye 0 0 0.2 0.4 0.6 0.8 1 Basic Salary Deduct PPF Ruzuku (Sh.bilioni) Chati 8: Tofauti kati ya ruzuku halisi iliyofika wilayani na Iliyopaswa kufika wilayani kwa mujibu wa MMEM II. vitabu. Lakini pia wazazi walidai hawashirikishwi na walimu, ili kuweza kufuatilia maendeleo ya elimu ya watoto wao, hivyo hawajui waanzie wapi. (HakiElimu, 2009) 

3.10 Vifaa vya maabara na vifaa vya sayansi bado ni changamoto kubwa maeneo mengi. Walimu wanaandaa masomo ya sayansi na kuyafundisha bila kuwa na vifaa vya kufanyia hivyo. Na baadhi ya vifaa hata vikipelekwa shuleni walimu hawajui kuvitumia wala kufundishia wanafunzi. Kwa sehemu kubwa walimu na wanafunzi walisema hakuna maabara, na hiki ni kikwazo kikubwa katika kufundishia masomo ya sayansi. Ni vigumu sana kufundisha masomo kama Biolojia, Kemia na Fizikia bila maabara na vifaa vyake. Wanafunzi10 walisema kwa kejeli kwamba hata “Bunsen burner” wanaijua kwa picha tu, lakini ngumu kabisa ni kujua matokeo ya uchanganyaji wa kemikali mbalimbali kwa njia ya kufikirika! 

3.11 Walimu wengi kukosa mafunzo ya ualimu kazini. Wengi wanashindwa kumudu kazi zao vizuri kwa sababu ya kukosa mafunzo hayo. Hasa walimu wa leseni ambao waliletwa kwa lengo la kusaidia kutoa elimu huku wakijiendeleza. Udhaifu wa walimu umezaa tatizo jingine pia la walimu kukataa baadhi ya masomo wanayopewa kufundisha. Na kutokana na hilo masomo kama Hisabati na Sayansi yana upungufu mkubwa wa walimu. Swala hili lilikuwa la utata kiasi kwani wakati, wilayani maafisa elimu waliripoti kuwa mafunzo kazini yamekuwa yakifanyika mara kwa mara, lakini kwa walimu wengi waliohojiwa walikanusha na kushangaa kuhusu suala hili. 

3.12 Uhaba wa vitabu na uwepo wa vitabu vya kiada vya waandishi tofautitofauti hasa shule za msingi unaathiri elimu nchini Tanzania. Maana wanafunzi wanachanganywa na uwingi wa vitabu hivyo. Na kibaya zaidi, vitabu hivyo vingi vina makosa. Kwa hiyo, kwa watoto wadogo wakifundishwa dhana moja kitofauti ni lazima watachanganyikiwa na kupoteza dira. Lakini kwa wilaya za vijijini suala kubwa ni uhaba wa vitabu vyenyewe kwenye maeneo mengi. Wauza vitabu na wasambazaji hawapeleki vitabu vyote, ni baadhi tu vitafika wilaya za pembezoni. Hali hii inasababisha baadhi ya shule kutoweza kupata baadhi ya vitabu hasa ambavyo wanaamini ni vizuri zaidi kwenye maudhui na uchambuzi wa mada. Na kwa sababu mtihani unatungwa mmoja nchi nzima, kutokuwa na usawa katika mgawanyo wa vitabu kunawapa faida ya upendeleo wanafunzi wa mijini wanaopata vitabu, na hivyo wanakuwa kwenye nafasi nzuri kufaulu zaidi mitihani kuliko walioko shule za vijijini. 

3.13 Wingi wa masomo shule za msingi ni tatizo kubwa kwenye baadhi ya maeneo yenye upungufu wa walimu na vifaa. Yaani mwanafunzi anakuwa na mzigo mkubwa na akimaliza 10 Sehemu ya mahojiano na wanafunzi katika shule mbalimbali za wilaya ya Monduli katika utafiti wa mahusiano kati ya ubora wa mitaala na elimu bora, Agosti 2010 hapo anakuwa hana stadi nyingi anazozimudu ili zimsaidie kujitegemea katika maisha. Walimu wanaona ni vyema huko mbeleni wanafunzi waelekezwe kwenye masomo machache tu na kwenye taaluma ambayo watakwenda nayo hadi ngazi za juu kisha itawasaidia kufanikiwa maishani. Ndivyo wanavyofanya wenzetu walioendelea. (Mtemi, 2011). 

4.0 Tufanye nini ili tuboreshe elimu yetu? 

Upatikanaji wa elimu bora unategemea mambo mengi sana, lakini, hapa tumejaribu tu kutaja mambo muhimu machache, kama mapendekezo ambayo yanaweza kuchangia kutoa dira. Uwepo wa mitaala bora na nyenzo bora za kufundishia na kujifunzia pamoja na ushiriki wa wadau muhimu katika michakato ya maendeleo na utekelezaji wa mtaala ni mambo muhimu sana ya kuzingatiwa. Utafiti wa HakiElimu na mashirika mengine, ikiwepo serikali pia umebaini kwamba shule nyingi hapa nchini hazina nyenzo bora za kufundishia na kujifunzia. Na mtaala wa taifa haukidhi tena mahitaji ya jamii pana. Ili kuboresha michakato ya maendeleo na utekelezaji wa mtaala, mapendekezo yafuatayo yametolewa:- 

4.1 Mitaala yetu inapaswa kuboreshwa ili ishabihiane na mahitaji ya jamii kubwa na mabadiliko makubwa yanayoendelea kutokea. Wananchi wengi wanaonekana kutaka kurudi kwenye mtaala unaoendana na elimu ya kujitegemea11, ili wahitimu waandaliwe kujitegemea na kumudu changamoto ndani ya jamii yao, hata kama watakosa fursa za kuendelea mbele waweze kuishi maisha ya ustawi. Wananchi na hata wanafunzi shuleni, wangependa kuona vijana wanapatiwa mafunzo ambayo yatawapatia ujuzi na maarifa ili waweze kujiajiri na kushiriki katika shughuli za kilimo, ufundi, biashara kwa kutumia mbinu za kisasa na za kuleta tija. 

4.2 Wananchi wengi wanadai kuwa mfumo wa matumizi ya vitabu vya aina nyingi hauna tija kwa kuwa unawafanya wanafunzi wajifunze dhana zinazotofautiana wakati wakitarajiwa wafanye mtihani wa aina moja12. Kwa mfano, iwapo kitabu kimoja kitasema, ini ni sehemu ya ubongo na kitabu kingine kikasema ini linapatikana tumboni maana yake ni kwamba watoto watakuwa wanachanganywa. Hii ni kuwadanganya watoto ukizingatia ukweli kwamba upatikanaji wa vitabu hivi hauko sawa (baadhi watapata A, wengine watapata B), lakini wote wanatarajiwa kufanya mtihani wa aina moja na wanatarajiwa kutoa majibu sahihi. Kwa kuwa Tanzania tumeamua kuwa na mtihani mmoja nchi zima, basi ni vema tukawa na vitabu ambavyo vinapatikana kwa usawa kwa shule zote, ili ushindani nao uwe wa usawa. 11 Elimu ya kujitegemea chini ya utawala wa Nyerere ndiyo iliyopandikiza fikra za watanzania kupenda kufanyakazi na kufanyakazi kwa ujumla. 12 Utafiti wa HakiElimu: Mahusiano kati ya ubora wa mitaala na Ubora wa Elimu, 2011 

4.3 Wananchi wengi, wazazi, walimu na wanafunzi walipendekeza matumizi ya vitabu vya aina moja, hasa shule za msingi. Na kwa hiyo serikali inapaswa kuliangalia hili kwa faida ya wote na ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na elimu bora na inayotolewa kwa usawa. Kwa hiyo, kuna haja ya kuifanyia marekebisho sera ya matumizi ya vitabu vya kiada iliyopo kwa sasa ili iwe kama ilivyokuwa zamani ambapo kitabu cha aina moja chenye ubora kilikuwa kinatumika nchi nzima. 

4.4 Ubora katika vitabu ni jambo nyeti na la muhimu sana. Vitabu ndiyo kiongozi kikubwa kwa walimu na wanafunzi hivyo waandishi wa vitabu hivi lazima wazingatie ubora na ukweli wa mambo. Wakati soko huria la utengenezaji na usambazaji wa vitabu lililenga kupunguza uhaba mkubwa wa vitabu, kuna haja ya kudhibiti ubora wa vitabu ili kuhakikisha kuwa vitabu vinavyopendekezwa kutumika mashuleni vinakuwa na ubora unaohitajika. Kwa sasa utafiti unaonesha, vitabu vinavyochapishwa na wachapishaji mbalimbali vinatofautiana sana kwa ubora na kwamba baadhi ya vitabu havina ubora unaohitajika. 

4.5 Ushiriki wa wazazi na wanajamii katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala ni suala muhimu katika kufanikisha kitendo cha ujifunzaji kwa wanafunzi. Kwa sasa ushiriki wa wazazi na wanajamii katika maendeleo na utekelezaji wa mtaala ni mdogo hapa nchini. Kuna haja ya kuchukua hatua madhubuti, kwanza kuwahamasisha wazazi na viongozi katika jamii juu ya umuhimu wa ushiriki wao katika maendeleo ya watoto wao shuleni. Pili, suala la mabadiliko ya mtaala ni sharti lizingatie maoni ya wadau wote muhimu ukijumuisha wazazi, walimu, wanafunzi na wanajamii wengine. Walimu na wazazi wana mchango mkubwa katika elimu na ni lazima wawe na uwezo wa kuchangia masuala mbalimbali ya elimu likiwemo la utunzi wa mitaala kwa nafasi na kiwango chao cha ujuzi. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa “wale wenye wajibu wa kufanya na vijana wa umri mdogo, wana nguvu kubwa zisizozidiwa na nguvu za yeyote yule kwa kutilia maanani hali ya baadaye ya jamii yetu. Nguvu hizi ziko katika makundi mawili, wazazi na walimu” (Agosti 27, 1966). 

4.6 Matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia katika shule za sekondari inaonekana kama kikwazo kikubwa katika ushiriki wa wazazi katika kuwasaidia watoto wao kwa kuwa wazazi wengi hawaimudu lugha hiyo. Suala la lugha ya kufundishia limekuwa likiibua mijadala mizito na kwamba mwafaka umekuwa haufikiwi katika suala hili. Kuna haja kwa Serikali kuchukua hatua madhubuti katika kuongoza majadiliano kuhusu lugha ya kufundishia katika mfumo wetu wa elimu ili kufikia muafaka. Watoto hujifunza vizuri zaidi iwapo wataimudu lugha ya kufundishia, vivyo hivyo kwa walimu wakati wa kufundisha. Suala hili linapaswa kutazamwa kwa makini zaidi ili kuhakikisha kuwa lugha ya kufundishia inafahamika vyema kwa walimu na wanafunzi. 

4.7 Ukosefu wa nyenzo na vifaa vya kufundishia na kujifunzia ulionekana kama kikwazo katika utekelezaji wa mtaala. Tatizo hili ni kubwa zaidi kwa vitabu vya sayansi na maabara. Ukosefu wa nyenzo hizi za kufundishia na kujifunzia hauwezi kupuuzwa kwa kuwa umebainishwa pia kwenye tafiti zilizopita. Kuna haja kwa wasimamizi katika sekta ya elimu kutilia mkazo suala la upatikanaji wa nyenzo za kutosha za kufundishia na kujifunzia katika shule zetu kwa kuwa bila upatikanaji wa nyenzo hizo muhimu ufanisi katika utekelezaji wa mtaala hautakuwepo. Wengi walikiri kuwa serikali imeamua jambo jema kupanua fursa za watoto wengi kupata elimu ya msingi na sekondari. Lakini waliongeza kusema kuwa, ni muhimu pia shule hizi ziwe bora na ni bora sasa kuboresha shule zilizopo na kuziwekea walimu wa kutosha, kuboresha mazingira ya kujifunzia, vifaa na vitabu, badala ya kuendelea kujenga shule nyingi ambazo hazina mafanikio. Tunarudia tena kunukuu maneno ya busara ya Mwalimu Nyerere, aliyewahi kusema kwamba, “.....tunaposema kupanua elimu ya sekondari, tunaharakisha sana kusema kwamba, watu watachangia ujenzi kwa juhudi zao, lakini majengo hayana umuhimu wa kwanza, ...vitu muhimu katika elimu ni walimu, vitabu kwa sayansi ni maabara” (The situation and Challenges of Education inTanzania, Nyerere 1984) 

4.8 Utekelezaji wenye ufanisi katika mtaala hutegemea mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia. Wanafunzi wengi walioshiriki katika utafiti walikosoa mazingira ya ujifunzaji. Japokuwa walimu walipongezwa na wanafunzi wengi, bado mazingira yao ya kazi ni magumu kwa kuwa wanafundisha madarasa makubwa, kuna ukosefu wa nyenzo za kufundishia, nyumba zao za kuishi siyo bora, mishahara yao ni midogo na hawapati mafunzo ya mara kwa mara. Kuna haja kwa wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na hatimaye kuwafanya watoto wawe na furaha, wawe salama. Shule inapaswa kuwa sehemu ambayo itawafanya watoto wafanikiwe kitaaluma na kimaisha. Hakuna ubishi kwamba, walimu wengi wamekata tamaa na ualimu imekuwa ni sehemu tu ya waliokosa, hivyo ni vema nchi ifanye jitihada za makusudi kurejesha upya hadhi na taaluma ya ualimu.

 4.9 Mafunzo kwa walimu: Kama kweli tunahitaji elimu bora hatuwezi kukwepa kuandaa walimu bora. Na walimu bora wanatokana na msingi bora wa mafunzo bora ya kutosheleza na yanayoendana na mtaala na dira za maendeleo za nchi. Walimu wakiandaliwa hovyohovyo watatoa elimu ya hovyohovyo-na hatimaye tutakuwa na wasomi wa hovyohovyo-wanaofanya kazi hovyohovyo na kuwa na maendeleo duni. Muda wa mafunzo kwa walimu tarajali lazima uwe kamilifu. Wakufunzi wao lazima wawe bora, na mafunzo kwa walimu kazini lazima yafanyike kwa ukamilifu wake bila kuleta visingizio vingi. Kama sekta nyingine wanapata semina, kozi fupifupi kwanini walimu wasipate hivyo. Hakuna njia ya mkato. Ili fedha inayotengwa na serikali kwenye elimu ilete tija basi mafunzo ya walimu ni muhimu ili kuandaa watekelezaji wazuri wa sera ya elimu. Na kwa sababu tayari Serikali ina Mkakati wa Usimamizi na Maendeleo ya Walimu (TDMS), ni muhimu mkakati huu utekelezwe kwa vitendo kama ulivyopangwa ili kusaidia kupunguza na hata kuondoa kabisa tatizo la walimu. 

4.10 Siasa – Ni lazima wanasiasa watambue kuwa sekta ya elimu siyo sehemu wala jukwaa lao la kuoneshana umahiri wa kuongea na kutoa maamuzi hata yanayotupeleka kuzimu. Wakati ni muhimu sana kwa viongozi wetu kuwa wabunifu na kuleta mawazo bunifu kuboresha sekta ya elimu, lakini pia wakumbuke wizara ya elimu inakuwa na mipango na bajeti yake kama wizara nyingine. Kabla ya kutoa maagizo kwa mashindano, ni lazima kuwe na uratibu na utekelezaji wa sera kikamilifu. Na mawazo ya kisiasa yazingatie na kufikiria athari za maagizo yasiyo na tija katika elimu. Mambo ya kitaalamu kuhusu elimu yashauriwe na wataalamu hasa walimu. 

4.11 Kuna mgawanyo usio sawa wa rasilimali za taifa hasa kwenye elimu. Shule za mijini zinaonekana kupendelewa kwa kila hali. Tafiti nyingi zinaonesha walimu wenye sifa wengi hupangwa mijini. Bado, hata mgawo wa ruzuku kwa wanafunzi shule za vijijini zinaonekana kupata kiasi na mara nyingi fedha zinachelewa kuliko shule za mjini13. Hii sio sawa. Watanzania wengi wako vijijini. Hivyo, ni lazima kuwe na mgawanyo sawa unaozingatia haki za watoto wote wa Tanzania. 

4.12 Kushangilia matokeo ya mitihani zaidi badala ya ujuzi na maarifa sio sahihi. Kila mtu anapenda kufanikiwa na kusifiwa, ndiyo hulka yetu binaadamu na hili si kosa. Watanzania tumeacha kushangilia tija sasa tunashangilia kufaulu mtihani, bila kujali tunapataje mafanikio hayo, kwa kuiba mitihani, ama kuweka mkazo mwaka wa mwisho tu (darasa la saba na Kidato cha nne) katika kufundisha. Tunapoteza nguvu nyingi sana kufundisha watahiniwa ili wafaulu mitihani na kutaka wilaya ama shule zetu ziongoze kwenye ufaulu , badala ya kutumia muda mwingi kuwasaidia watoto kupata maarifa, ujuzi na ubunifu ili uwasaidie maishani. 

4.13 Kwa nini tusijiulize swali, kwanini baadhi ya watoto wetu wanafaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari lakini hawajui kusoma na kuandika vizuri? Je hii ni elimu na mafanikio ya kushangilia? Elimu siyo cheti, bali ni uwezo, kama mwalimu Nyerere alivyowahi kusema, 13 MOVET –PETS 2009 na HakiElimu PETS 2010 ..“kinyume kabisa na elimu, ni aina ya mafunzo inayomfundisha mtu kujifananisha na bidhaa, ambazo thamani yake inapimwa kwa vyeti, shahada, au sifa nyingine za kitaaluma”(Nyerere 20 Mei 1974) 

4.14 Kiuhalisia, elimu ya kweli hupatikana kwenye mchakato unaoendelea kati ya mwalimu na mwanafunzi darasani. Hivyo, mbinu za kufundishia na vitendo vya ujifunzaji vinapaswa viboreshwe kikamilifu. Kazi za kujifunza darasani na mbinu za kuibua vipaji na kuchagiza maarifa ni muhimu viboreshwe. Na walimu wanapaswa kuwa na hamasa ya kufanya hivyo ili tupate manufaa ya haraka. 

4.15 Mazingira mazuri ya kazi ndicho kigezo muhimu zaidi kinachoamua kiwango cha moyo wa kujitolea walio nao walimu katika kufundisha, na matokeo yake kigezo hiki huwa na nguvu sana katika kuleta matokeo mazuri ya wanafunzi kitaaluma. Bila kurekebisha hili uwekezaji mkubwa katika elimu hautaleta tija katika taaluma ya ualimu na elimu kwa ujumla 

4.16 Mwalimu kuwa na sifa nzuri za kitaaluma pekee yake bila moyo wa kujitolea haitosho kuimarisha ufaulu wa mwanafunzi. Shule zenye walimu wenye moyo wa kujitolea wa hali ya juu bila kujali iwapo walikuwa na sifa za juu kitaaluma (shahada au zaidi) au la zilifanya vizuri katika mitihani ya taifa. Jitihada mahsusi zifanyike kurejesha hamasa, kujituma na moyo wa kufundisha. 

4.17 Serikali na wadau wengine washirikiane kuboresha mazingira ya kazi na makazi ya walimu. Usimamizi thabiti kuhakikisha kuwa walimu wanatimiza wajibu wao, hii itasaidia kujituma zaidi na kuleta ufanisi katika kazi. Maslahi ya walimu yaboreshwe, na pia walimu wapandishwe madaraja na kulipwa stahili zao bila kucheleweshwa; hii itachangia kurejesha hamasa. Na Mafunzo kwa walimu kazini ya uongozi kwa wakuu na wasimamizi wa shule yatolewe kwa ukamilifu na mara kwa mara, kwani yatasaidia sana kuongeza ufanisi na ufundishaji wa walimu

 4.18 Vigezo vitumike bila upendeleo au woga kuhakikisha kwamba kila shule inafikia viwango vinavyokubalika ndiyo ifunguliwe na iendeshwe kama shule; shule ziwezeshwe kufikia viwango hivi; na zile ambazo zitashindwa kwa kipindi kilichokubaliwa zisiruhusiwe kuendelea ‘kupotosha’ ama ‘kupotezea’ muda wanafunzi. Zifungwe kama zinavyofungwa zahanati zisizofikia viwango kubalifu. 

4.19 Jitihada mahsusi za baadhi ya walimu zitambuliwe na walimu hao watuzwe ili kuwatia moyo, na kuwahamasisha wengine kufanya kazi yao kwa bidii. Kujituma na kuwajibika ni sehemu muhimu ya maadili ya walimu, hivyo inawapasa walimu wote nchini wazingatie hili; hata kama wakiwa na hoja ama madai mengine ya msingi. 

5.0 Hitimisho 

Nchi haiwezi kuendelezwa na watu wachache wanaopata fursa za kipekee kwenye shule chache huku elimu ya jamii pana ikiwa mashakani. Hakuna haja kulumbana wala kuingiza siasa katika elimu, bali serikali itekeleze mipango na sera zilizopo na kuboresha mapungufu kwa kushirikisha wadau. Na ukweli wa hali ya elimu nchini usisulubiwe wala kubezwa bali tuupokee na kuuwekea mikakati kwa pamoja tuweze kuboresha elimu yetu. Pa kuanzia ni kila mmoja katika eneo lake, na kikubwa kufanya zaidi ya mazoea.


TEACHERS AND STUDENTS;- MPANGO MPYA WA ELIMU

Ungana na FARAJA KOTA



  • Kutana na Maelfu ya wanafunzi wa sekondari katika kila mkoa wa TANZANIA.  

  • kwa kutembelea webiset yao  www.shuledirect.com itakayo kuwezesha wewe kama mwanafunzi kujisomea notes mbali mbali, kujadiliana na wanafunzi mbali mbali na pia kuuliza maswali kwa waalimu walobobea katika masomo mbali mbali.

  • wewe kama mwalimu pia unakaribishwa kujiunga na walimu wenzako ili uwezesha elimu ya TANZANIA kusonga mahala panapo hitajika.

  • kujisajiri ni bre kabisa tembela website ya SHULE DIRECT ambayo ni www.shuledirect.com ili upate kujisajiri..


  • pia waweza uka follow facebook page ya SHULE DIRECT yenye jina Shule direct.




STUDENTS

STUDENTS.

Thursday, 2 June 2016

QUALITY OF EDUCATION IN TANZANIA- STATISTICAL

Poor quality education is eating away at Tanzania’s skills base, denying the country the human capital it needs to grow.


A survey, which revealed that secondary education is headed for a crisis, has put the spotlight on the government.
Twaweza, an education-focused think-tank, released the results of the survey, which indicate that parents largely blame the government and teachers for the decline in standards.
The survey showed that based on student learning assessments, mathematics and English reading competence levels are disturbingly low, confirming the national examination results released in February.
The results showed six out of every 10 students who sat last year’s National Form Four examination in Tanzania failed. Only 126,851 passed the examination out of the 397,132 who attempted it. In 2011, 53.6 per cent passed, and 50.4 per cent passed in 2010.
The survey shows that 72 per cent of sampled primary school students and 66 per cent of secondary school students could not carry out a multiplication test meant for Class 2. Moreover, a large majority of students in primary school could not answer a comprehension question for a story in English or Kiswahili.
The inability of students in secondary schools to comprehend a Standard 2 level story in English, when English is the language of instruction, is troubling, Twaweza said. It paints a grim picture of literacy and numeracy skills in Tanzanian schools as it shows children in schools are not learning.
“The massive investment in education in the past decade has not yet translated into learning gains for students. The government will need to review evidence of what drives learning and adjust its policies, programmes and goals accordingly. Transforming teacher motivation, effectiveness and accountability are at the heart of this challenge,” said Twaweza in the May 15 survey.
Respondents overwhelmingly perceived a decline in the quality of secondary education over the past 10 years, with about 8 out of 10 citizens (83 per cent) indicating that they felt education had deteriorated. This is consistent with official statistics including the Ministry of Education’s Basic Education Statistics in Tanzania.
Results released by the Ministry showed there was massive failure in last year’s Form Four examinations, which saw the government nullify the results and order a fresh rating.
When probed further, parents reported a shortage of textbooks for their children. At primary level, nearly 6 out of 10 parents (55 per cent) report that their children have no textbooks; at secondary level, some 5 out of 10 (54 per cent) said that their children have two or more textbooks. However, secondary school students are expected to have a minimum of one textbook per subject for between six and nine subjects.
“Parents are clearly aware that the education system is failing their children. They are trying to play an active role in their children’s education and are asking teachers and the government to do the same,” said Elvis Mushi, a researcher at Twaweza.
A quarter of the parents interviewed said the government must increase the number of teachers in schools to boost the quality of learning while 17 per cent said the government must work towards improving the quality of teachers.

OUR OBJECTIVES.


HOW ARE WE GOING TO ACHIEVE OUR AIMS?



1. To collaborate and network with potential partners among NGOs, donors and other institutions, in order to mobilize resources to address the needs and concern of the disadvantaged civil society.

2. To reduce child labor through access to quality education, particularly for girl children in poor and rural communities.

3. To advocate for the interest and concerns of the civil society, disadvantaged youths and young people, women, and children who are voiceless and defend their fundamental human rights to be heard.


OUR AIMS.


OUR AIMS.



The major aim of this  foundation is individuals o stand  as whole in helping people who are in needs. The description is as follows:-


1. making sure that each Tanzanian students get better education. Whereby the foundation will help all students from different institutions  who are in need of help, Eg, Books, clothes, desks and chairs,  and all needed learning materials for those who are in need.

2. Making sure that each Tanzanian woman get special care during the delivery of child. This is to mean that the foundation will have to provide all needed equipment to facilitate the whole process.

3. the foundation will stick it’s basis towards  the social development in a given society.

4. Natural environment; support for the enhancement of horticulture, trees & forests .

5. Arts; supporting young/emerging creative artists, writers  in communities.

6. also the foundation aimed  to instill human rights norms and values as inalienable rights within the disadvantaged societies  in Tanzania.




Saturday, 14 May 2016